WATUHUMIWA WATATU WA USAFIRISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA WASAFIRISHWA KWENDA MAREKANI KUTOKANA NA USHIRIKIANO IMARA WA KIUSALAMA KATI YA MAREKANI NA TANZANIA


Ubalozi wa Marekani
Dar es Salaam
TANZANIA
03 Mei, 2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Dar es Salaam, TANZANIA. Hapo tarehe 1 Mei 2017, mtuhumiwa wa usafirishaji wa madawa ya kulevya Ali Khatib Haji Hassan (“Shkuba”) na washirika wake wawili Iddy Salehe Mfullu na Tiko Emanual Adam walisafirishwa kwenda nchini Marekani, kukabili mashtaka yao kuhusiana na biashara haramu ya madawa ya kulevya katika Mahakama kuu huko Huston, Texas. Watuhumiwa hao watatu waliwasili nchini Marekani tarehe 2 Mei 2017. Kusafirishwa kwa watuhumiwa hao ni matokeo ya ushirikiano mkubwa, wa karibu na wa muda mrefu baina ya serikali za Marekani na Tanzania.
“Kupelekwa nchini Marekani kwa Hassan na washirika wake ni mafanikio yatokanayo na ushirikiano wetu wa muda mrefu na wenzetu katika serikali ya Tanzania katika nyanja nyingi katika sekta za usalama, usimamizi wa sheria na haki. Kesi hii ni mfano mzuri sana wa jinsi tunavyoweza kuimarisha usalama wa kikanda na kimataifa pale tunapofanya kazi pamoja,” alisema Virginia Blaser, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania na katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

No comments:

Post a Comment