WATUMISHI 6 JELA KWA VYETI FEKI


Maregesi Paul-Dodoma na ALLY  BADI- KILWA
UAMUZI wa Serikali wa kuwafukuza kazi watumishi wanaodaiwa kughushi vyeti, umezidi kuchukua surampya, baada ya watumishi sita wa Halmashauri ya Kilwa mkoani Lindi kufungwa jela mwaka mmoja kila mmoja kwa kosa la kughushi vyeti vya kidato cha nne na kujipatia ajira.
Taarifa nyingine zinasema Katibu Tawala wa Wilaya ya Tandahimba (DAS), Mohamed Azizi naye ameguswa na sakata la vyeti feki baada ya kutajwa katika orodha ya watumishi wenye vyeti feki akiwa namba 5356.
Chanzo cha uhakika kutoka ofisi ya DAS kimelidokeza MTANZANIA kuwa, tayari kiongozi huyo ameshaondoka Mtwara kuelekea Dar es Salaam kupeleka malalamiko yake katika mamlaka za juu kwamba jina lake limeingizwa kimakosa katika orodha hiyo.
Taarifa nyingine kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini zinasema zahanati mbili zimefungwa baada ya watumishi wote waliokuwapo kukumbwa na sakata la vyeti feki.

No comments:

Post a Comment