DREAMLINER YAANZA KAZI KWA KUFANYA SAFARI ZA NDANI

Wakuu wa mikoa sita jana, walikuwa miongoni mwa wageni walioipokea ndege mpya aina ya Boeing 787-8 kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mangola wakuu wa mikoa walishuhudia ndege hiyo ya kisasa, ikitua kwa mara ya kwanza mjini hapa saa 4:19 asubuhi ikiwa na abiria 255.

Wakuu wa mikoa hiyo, Adam Malima (Mara), Mhandisi Robert Gabriel (Geita), Zainabu Tarack (Shinyanga), Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu (Kagera) na na Anthony Mtaka (Simiyu) na viongozi dini

Akizungumza wakati wa mapokezi ya ndege hiyo,Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwele alisema Serikali ina mpango wa kuboresha majengo ya abiria na mizigo ikiwa ni pamoja na upanuzi wa viwanja vya ndege nchini.

No comments:

Post a Comment