Umoja wa Ulaya watoa kauli mpya kwaTanzania

Dar es Salaam. Umoja wa Ulaya (EU) umesema unasikitishwa na hali ya kuendelea kuzorota kwa haki za binadamu na utawala wa sheria nchini na kwamba utafanya mapitio mapana ya uhusiano wake na Tanzania, kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa kwenye tovuti ya umoja huo.


Hali hiyo imekukuja baada ya EU kumrejesha balozi wake nchini, Roeland Van de Geer makao makuu yake yaliyopo Brussesls, Ubelgiji kwa ajili ya mashauriano.

Katika kipindi ambacho Van de Geer hatakuwepo, taarifa imesema naibu wake Charles Stuart atatekeleza majukumu yake kama mwambata wa shughuli zote.

Aliondoka Jumamosi saa 5:55 usiku kwa ndege ya Shirika la KLM kupitia Amsterdam, Uholanzi.

Lakini Serikali imesisitiza kuwa haikumfukuza mjumbe huyo badala yake imesema uamuzi wa kumrejesha ulifanywa kwa majadiliano ya pamoja na mamlaka kutoka pande zote mbili.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Augustine Mahiga alisema mjumbe huyo aliitwa makao makuu ya EU na kwamba serikali ilijadili suala hilo.

"Amerudishwa EU ambako labda kuna kazi nyingine au majukumu mengine kwa ajili yake. Ameitwa na wala hakufukuzwa na ni jambo la kawaida kuitwa na serikali yake (mwajiri)," alisema Mahiga.


Soma Zaidi:

No comments:

Post a Comment