Papa ameyasema hayo katika Ibada ya Misa ya mkesha wa Krismasi ndani ya Kanisa la Mtakatifu Petro mjini Vatican, misa ambayo ni moja ya sherehe muhimu zaidi za Kikatoliki katika kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
”Kuzaliwa kwa Kristo kunamaanisha njia mpya ya kuishi nayo si kwa kuharibu na kutumia mali nyingi kwa kusherehekea lakini kwa kugawana na kutoa kwa kila mwenye uhitaji”, amesema Papa Francis.
Papa pia amesisitiza kuwa ”chakula cha maisha si utajiri wa mali lakini upendo, si uovu lakini upendo, si uchafu lakini urahisi na hiki ndicho humpenda Mungu”.
Leo mchana atatoa ujumbe wake wa sita wa Urbi et Orbi tangu alipochukua wadhifa huo. Mara nyingi ujumbe wa Urbi et Orbi hutumiwa kuomba amani ulimwenguni na hutolewa wakati wa Siku Kuu ya Pasaka, Krismasi na baada ya kuchaguliwa kwa Papa.
No comments:
Post a Comment