MNAOCHAGUA WA KUWAOA SOMENI HII

ZAMA hizi ni za kusaidiana kwa kila kitu. Kama wewe ni binti ambaye unatamani na unataka ukute au upate mwanaume wa kukuoa akiwa na kila kitu bila wewe kuvuja jasho au kushiriki, utasubiri sana. Utaendelea kulalamika kuwa hakuna waoaji bila kujua waoaji wapo lakini nao wana vigezo vyao. Waoaji wapo ila wewe una ubaguzi, una matabaka, unataka usiangaishe akili yako kufikiria kuhusu mafanikio bali unataka mafanikio yaliyo tayari. Ni tatizo! Kama una tabia na fikra za aina hiyo wewe ni mwanamke ambaye ni tegemezi, hata kama ukipewa mtaji wa milioni bado unaweza kuumaliza kwa fikra kuwa wakukupa mtaji mwingine yupo.

Kama wewe unachagua mwanaume mwenye kazi, nyumba nzuri, gari na mshahara, elewa kuwa hata wanaume nao wanahitaji na wanachagua mwanamke mwenye kujitambua, mwanamke mwenye kujisimamia. Wanataka mwanamke mwenye kazi, mwanamke ambaye anaweza akasimama yeye mwenyewe hata kama mwanaume atakuwa kwenye matatizo ya kiuchumi au kiafya.

Kwa sasa hakuna mwanaume ambaye anapenda kuoa au kuwa na uhusiano na mwanamke ambaye yupoyupo, hana kazi. Japo kuna wanaume wengine wanaopenda wanawake wao wasifanye kazi, lakini kwa ujumla wake na hali ya sasa, wengi wana-tamani yule ambaye atape-nda kujishu-ghu-lisha.

No comments:

Post a Comment