Mnaotamani watoto kwa nguvu, hii inawahusu!




KADIRI miaka inavyozidi kuyoyoma, wimbi kubwa la wanawake kutaka kuzaa limezidi kuongezeka. Hii inatokana na suala zima la umri. Mwanamke akiona umri unamtupa mkono, haraka sana anahaha kusaka mtoto. Utasikia; ‘bora na mimi hata nizae tu niache angalau chata hapa duniani.’ Suala hili pia lipo kwa wanaume lakini kwa asilimia kubwa linawatesa sana wanawake. Wanapoona miaka inakatika, wanakimbilia kuzaa bila hata ya kuangalia anazaa na nani.

Anazaa tu ili mradi naye aitwe mama. Wapo wengi ambao sasa hivi pia wanaamua kuzaa kwa kufuata mtindo wa sasa kwamba hawataki stress. Mwanamke anasaka maisha yake, anaona anajimudu hivyo hataki kushirikiana na mwanaume sababu atamuongezea matatizo. Sasa hivi wengi najua ni mashahidi wa hili. Wanawake wengi ukizungumza nao, wanakwambia hawataki kuishi na mwanaume. Wanasema eti ni wasumbufu na wao hawataki usumbufu. Hivyo anaamua kuzaa na mwanaume ambaye hata hana mwelekeo wowote wa maisha. Ili mradi tu ampatie mtoto halafu yeye andelee na maisha yake.

Hataki kusikia habari za kubanwa na mwanaume kwamba uko wapi, unafanya nini au kwa nini umechelewa kurudi nyumbani. Anataka ashindane na wanaume wanaochelewa kurudi nyumbani kutokana na majukumu mbalimbali ya kikazi. Akiamua kurudi nyumbani alfajiri, sawa

No comments:

Post a Comment