Madhara ya Wapenzi Kugombana na Kununiana Mara kwa Mara

MWISHONI mwa wiki iliyopita, nilipata bahati ya kukutana na mmoja kati ya wasomaji wangu wa siku nyingi ambaye amekuwa akiufuatilia ukurasa huu na kujifunza mambo mbalimbali.

Alikuwa na shida iliyomfanya anitafute na alichonieleza, ni kwamba alikuwa akiujutia moyo wake kwa sababu alikuwa amemfanyia kosa kubwa mume wake kwa sababu ya hasira na sasa nafsi yake ilikuwa ikimsuta.

Kibaya zaidi, dhambi aliyokuwa ameifanya, ilikuwa imemnogea kiasi cha kuhatarisha ndoa yake. “Mimi na mume wangu tumekuwa tukigombana mara kwa mara na kibaya zaidi ni kwamba tunapogombana, inachukua muda mrefu sana kumaliza tofauti zetu. Wakati mwingine tunakaa hata mwezi mzima tukiwa tumenuniana ndani ya nyumba, yaani hata salamu hakuna.

“Miezi michache iliyopita, mimi na mume wangu tuligombana na hiyo ilikuwa ni baada ya mimi kukuta meseji kwenye simu yake, ambayo inaonesha inatoka kwa mwanamke ambaye wana mazoea ya kupitiliza. Nilipomhoji, alinijia juu na ugomvi mkubwa ukazuka kati yetu na tukanuniana kwa muda wa wiki mbili.

No comments:

Post a Comment