TAARIFA MUHIMU KUHUSU PASSPORT KWA WATANZANIA WAISHIO MAREKANI

Image result for PASSPORT MPYA ZA TANZANIA
Unataarifiwa kwa wale wote ambao Pasi za kusafiria zimeisha muda wake mnaombwa kuzibadilisha na kupata pasi mpya.

INASHAURIWA Usisubili dharula itokee badilisha Passport yako sasa, hata kama ni hati ya dharula ya kusafiria huchukua siku 3 mpaka 4 kua tayari.

Kila kitu kinafanyika matandaoni, kwa taarifa zaidi tembelea tovuti ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico www.tanzaniaembassy-us.org . Fomu za passport na za hati ya dharura zinajazwa kupitia www.immigration.go.tz sehemu ya e-services.Fomu ya maombi iliyokamilika na nyaraka zote ikiwa ni pamoja na cheti cha kuzaliwa ama affidavit, cheti cha kuzaliwa ama affidavit ya mzazi mmoja wapo, nakala ya passport na nakala ya kitambulisho vinapokelewa ubalozini kupitia barua pepe ubalozi@tanzaniaembassy-us.org. Tafadhali pitia viambatisho vya maelekezo kwa uelewa zaidi hapo chini.

Kwa taarifa zaidi na maelekezo USISITE wasiliana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Washington, DC simu 202 884-1080 ASANTE.

No comments:

Post a Comment