WENGINE NAO MAJINA YAO YATAJWA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA HELKOPTA

Image result for kobe bryant
TAARIFA za vyombo vya usalama nchini Marekani zinasema kuwa waliofariki mpaka sasa katika ajali ya helikopta iliyotokea jana huko Los Angeles, Marekani, ni Kobe Bryant, mwanaye Gianna Maria Onore, rafiki wa mwanaye, Alyssa, ambaye aliambatana na wazazi wake John Altobelli na Keri.

Wengine ni kocha wa Gianna na Alyssa kwenye kituo cha kufundisha mchezo wa mpira wa kikapu cha Kobe anayefahamika kama Christina Mauser, abiria wengine ni Sarah na Payton Chester na rubani Ara Zobayan.

Maelfu ya watu wamefurika nje ya uwanja wa nyumbani wa Los Angeles Lakers, Staples Center muda mfupi baada ya kutokea kwa kifo hicho, kila mmoja akimuenzi Kobe Bryant kwa namna yake.
 
Katika kituo cha Mamba Sports Academy, wachezaji watoto wote walikuwa wakisubiri kocha wao Christina Mauser, mlezi na kocha wao Kobe Bryant waje na wachezaji wawili ambao ni Gianna na Alyssa kwa ajili ya mchezo uliokuwa unafuata.

No comments:

Post a Comment