MBOWE AVAMIWA USIKU JIJINI DODOMA

DAR ES SALAAM: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kinahitaji uchunguzi wa uhuru katika tukio la kuvamiwa kwa mwenyekiti wao, Freeman Mbowe.

Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari leo jijini Dar, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alianza kwa kuthibitisha tukio hilo kwa kusema Mbowe alivamiwa usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana wakati akiwa anaingia nyumbani kwake jijini Dodoma.

Alisema, baada ya shambulio hilo alikimbizwa kwenye Hospitali ya Ntyuka jijini Dodoma na kwamba bado anaendelea na matibabu lakini wanafanya utaratibu wa kumsafirisha hadi jijini Dar kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.

Mnyika alilitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi kwa uhuru ili waliohusika na jambo hilo wafahamike kwa haraka na kuchukuliwa hatua stahiki.

“Taarifa ya kamanda wa polisi imetoa viashiria kwamba kama ilivyokuwa kwa tukio la kupigwa risasi kwa mheshimiwa Tundu Lissu ambapo polisi walijitokeza harakaharaka, katika tukio hili pia wamejitokeza harakaharaka wakitaka kwa namna yoyote lisihusishwe na siasa.

“Kwa sababu wamesema wanafanya uchunguzi hawapaswi kufunga milango ya uchunguzi na kuliita hili tukio la kawaida kwa sababu tukio hili lina viashiria vya kisiasa kwani taarifa zinaeleza wakati wanamshambulia walisikikika wakisema ‘tuone utafanya vipi hizo kampeni’,” alisema Mnyika na kuongeza.

“Waliomshambulia Mwenyekiti Freeman Mbowe kuna maneno walikuwa wanayatamka zaidi ya haya ya kwamba wewe unaisumbua sana Serikali, walikuwa wanasema kwamba hatudhamirii kukuuwa lakini pamoja na kutamka maneno hayo walikuwa na silaha ambazo hawakuzitumia

No comments:

Post a Comment