ASKARI ACHOMWA MKUKI WA UBAVU MARA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Ernest Mangu
Baadhi ya picha za matukio ambayo jeshi la polisi hupamba nayo.

Na Samson Chacha - Mara
Askari polisi Deogratius wa Kituo cha Polisi, Kinesi Wilayani Rorya mkoani Mara, amechomwa mkuki na wananchi waliovamia mgodi wa dhahabu wa ACACIA North Mara kwa lengo la kupora mawe.

Kamanda wa Polisi wa Tarime Rorya, ACP Lazaro Mambo, alisema jana kuwa, askari huyo alijeruhiwa na kundi la watu zaidi ya 2,000 lililovamia kwenye mgodi huo Jumanne ya wiki hii.

Alisema wavamizi hao walikuwa na silaha mbalimbali za jadi.
Alisema mara baada ya kuingia ndani ya mgodi huo, watu hao walifanya vurugu kwa kuwashambulia askari na walinzi waliokuwa wakilinda mgodi huo.

No comments:

Post a Comment