TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSIANA NA TAHARUKI YA PANYA ROAD

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ndugu zangu wanahabari;
Napenda nichukue fursa hii kutoa ufafanuzi wa taharuki iliyotokea jana tarehe 02 Januari, 2015 katika jiji la Dar es Salaam ikiwahusisha baadhi ya vijana wanaojikusanya kwenye vikundi na kujiita Panya road na pengine kusababisha hofu kubwa kwa wananchi.
Chanzo cha taharuki hiyo, kulitokana na kuuawa kwa kijana mmoja ajulikanae kwa jina la Mohamed Ayub na wananchi tarehe 01/01/2015 katika maeneo ya Tandale kwa Mtogole kwa tuhuma za wizi wakati wa mkesha wa sikukuu ya mwaka mpya. Tarehe 02/01/2015 majira ya saa tisa mchana yalifanyika mazishi ya kijana huyo katika makaburi ya Kihatu Kagera Mikoroshini na taarifa zilizokuwa zimelifikia Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam ni kwamba baada ya mazishi hayo…

No comments:

Post a Comment