TABIA HII YA WAUZA MITUMBA SOKO LA MCHIKICHINI NI UDHALILISHAJI WA KIJINSIA

Baadhi ya wateja wa nguo wakichagua nguo kwenye soko la Mchikichini

Baadhi ya wateja wa nguo wakichagua nguo kwenye soko la Mchikichini jijini Dar es Salaam.

Na Andrew Chale wa Modewji blog
Miongoni mwa mambo ya aibu katika jamii ni pamoja na masuala ya udhalilishaji wa kijinsia ukiwemo ule wa maungoni hasa kwa wanawake.
Kwa muda mrefu mtandao huu umekuwa ukifuatilia vitendo hivyo vibaya kwa jamii vinavyofanywa na watu waliokosa ustaarabu hasa jamii ya vijana katika maeneo ya mikusanyiko ya watu wengi karibu maeneo mengi ikiwemo jiji la Dar es Salaam.
Miongoni mwa eneo linaloongoza kwa kuwadhalilisha wanawake ni eneo la soko la Mchikichini lililopo Ilala Mkoa wa Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment