Adha ya Mbweni JKT, Kinondoni

Ukiwa na haraka Mbweni JKT jiandae kupiga mbizi


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UPIGE mbizi. Ndivyo unavyoweza kusema msemo huu kama unahitaji kupita haraka haraka katika eneo la Mbweni JKT, wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam, mahala panapojengwa daraja la kuvukia watu kwa miaka mitatu sasa, halina dalili za kukamilika hivi karibuni. Ni eneo tata. Ni eneo linalokera na kusumbua watu mno. Mbaya zaidi, ni eneo lililozunguukwa na majumba ya watu wenye ukwasi au ukubwa wa majina ya viongozi waliojenga katika eneo hilo. Eneo linalojengwa daraja hilo ni kwenye mkondo wa maji unaotokea baharini.
Gari likivuka eneo la mkondo wa bahari, ambapo pia ndipo panapojengwa daraja hilo hatua chache mkono wa kulia kutoka gari linapopita. Maji yakijaa hapo hakuna kupita wala kuvuka.

Kwa wanaofahamu tabia za mikondo hii ya baharini watakuwa wanaelewa. Na wasiofahamu ni kwamba, linakuwa na tabia za kujaa maji na kupungua kila wakati. Kwa mfano, mtu anaweza kupita saa tatu asubuhi akakuka hakuna maji mengi. Lakini dakika kadhaa mbele, maji mengi yanajaa kutokea baharini. Ukifanya mkosi, ukiwa na haraka ya kuendelea na shughuli zako, ndipo hapo unapopaswa upige mbizi.
Hapa ndipo panapojengwa daraja hili.

Uyavulie nguo, upite. Na ikiwa na una gari, huna budi kusubiri kwanza yapunguwe kama si kuisha kabisa maji hayo. Au utafute njia nyingine za kukufikisha eneo unaloelekea, ingawa njia hiyo ina usumbufu mkubwa wa muda na gharama nyingine pia. Ni kutokana na hilo, serikali kwa kupitia Halmashauri ya Wilaya Kinondoni, inapaswa kupigia jicho kuu eneo 

No comments:

Post a Comment