Kinara uporaji benki Mbagala mbaroni.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro.

Siku nne baada ya majambazi 12 kuvamia Benki ya Access tawi la Mbagala, jijini Dar es Salaam na kuiba Sh. milioni 20 na kusababisha vifo vya watu sita, mtu anayedaiwa kuwa kinara wa uhalifu huo ametiwa mbaroni baada ya kutajwa na washirika wake, akiwamo aliyekamatwa akiwa anafunga ndoa.

Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili ilizipata zinaeleza kuwa, kinara wa ujambazi huo alikamatiwa Sinza Mori, wilaya ya Kinondoni jana, saa 11:00 jioni.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Nipashe ilizipata, kikosi kinachoshirikisha askari wa majeshi mbalimbali ikiwamo, polisi na la wananchi wa Tanzania, kilinasa watu wanne kwenye sherehe ya harusi baada ya kufuatilia mawasiliano yao ya simu.

No comments:

Post a Comment