Kamishna wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na wanachi wa maeneo ya Manzese, wakati akitoa elimu ya Ulinzi na Usalama Jijini.
Sehemu ya Wananchi walioitikia wito wa Kamanda Sirro, alipokuwa akitoa somo kuimarisha ulinzi na Usalama Jijini.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro ameamua kuingia mtaani na kutoa elimu ya Ulinzi na Usalama Jijini huku akiwataka wananchi wanaotumia nyumba za ibada kujifunza mambo ya kivita waache mara moja maana inahatarisha amani ya nchi na kuongeza kuwa jambo hilo ‘halilipi’ hata kidogo badala yake wafanye shughuli zinazoweza kuwaingizia kipato na kuongeza uchumi wao.
Kamanda Sirro ametoa wito huo leo alipokuwa akiongea na wananchi katika katika maeneo ya Manzese, jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za kuimarisha ulinzi na usalama jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment