WATU 14 WAFARIKI DUNIA KWA UGONJWA UNAOSABABISHWA NA SUMUKUVU

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu

Hussein Makame-MAELEZO
Watu 14 wamefariki dunia katika wilaya za Chemba mkoani Dodoma na Kiteto mkoani Manyara kutokana na ugonjwa unaojulikana kitaalamu kama ‘Aflatoxicosis’ unaosababishwa na sumu kuvu (Aflatoxins) kwenye nafaka iliyoharibika.

Hayo yamesema na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya magonjwa ya milipuko na magonjwa mengine leo jijini Dar es Salaam.

“Ugonjwa uliosababishwa na sumu kuvu (Aflatoxins) uliripotiwa kwa mara ya kwanza tarehe 13 Juni, 2016 katika wilaya za Chemba mkoani Dodoma na baadaye mkoani Manyara katika wilaya ya Kiteteo” alisema Waziri Ummy na kuongeza kuwa: 

“Wagonjwa walikuwa na dalili za kuumwa tumbo, kuharisha, kutapika, tumbo kuvimba na kuwa manjano sehemu mbalimbali za mwili ambayo inaashiria kuathirika kwa ini”

Alisema mbali na vifo hivyo, hadi kufikia Julai 31 mwaka huu wagonjwa 54 waliripotiwa kuugua ugonjwa hu huku wagonjwa wanne wakilazwa kutokana na kuugua.

No comments:

Post a Comment