Whatsapp Yafutwa China

Baada ya malalamiko ya muda mrefu ya serikali ya China juu ya mtandao wa ujumbe mfupi wenye kubeba mafaili ya Sauti, Picha na Video “WhatsApp” hatimaye imeuondoa rasmi nchini humo.

Imeripotiwa kuwa mtandao wa WhatsApp haupatikani nchini China kwa siku ya tatu sasa ambapo inadaiwa kuwa Mamlaka ya Mawasiliano nchini humo 'Observatory of Network Interference' (OONI) imefuta matumizi ya mtandao huo.

WhatsApp ambayo inamilikiwa na kampuni ya Facebook yenye makao yake makuu nchini Marekani imekuwa kwenye mgogoro na China ikilalamikia Serikali na mamlaka za usalama nchini humo kuingilia mawasiliano ya wateja wao kwa madai ya kufanya uchunguzi wa usalama wa taifa.

Hata hivyo kwa wageni wanaoingia nchini China huduma hiyo bado inapatikana kupitia SIM Card za mataifa yao hivyo inaonekana huduma hiyo imesitishwa kwa raia wa China pekee.

No comments:

Post a Comment