MOROGORO WASHEREKEA MKESHA WA MWAKA MPYA KWENYE MAFURIKO


Mvua kubwa zilizonyesha kwa muda mfupi mjini Morogoro zimesababisha mafuriko baadhi ya barabara kushindwa kupitika na maji kujaa katika baadhi ya maduka.
Wakazi wa mji wa Morogoro wakizungumzia mafuriko hayo wamelalamikia miundombinu mibovu ya barabara kutokana na kuziba kwa mitaro ambapo wameitaka halmasauri ya mji wa Morogoro kuzibua mitaro hiyo huku baadhi ya wafanyabiashara wakilalamikia kupata hasara.

No comments:

Post a Comment