MAHAKAMA YAMVUA KENYATTA MAMLAKA KUTEUA JAJI MKUU
Mahakama Kuu ya Kenya imebatilisha marekebisho ya sheria yaliyompa Rais mamlaka ya kuteua Jaji Mkuu kinyume na Katiba, uamuzi ambao umeelezewa na wanasheria wa Tanzania kuwa umechelewa kufanywa hapa nchini.
Wiki iliyopita, majaji watano wa Kenya, Richard Mwongo, Joseph Onguto, George Odunga, Weldon Korir na Mumbi Ngugi walibatilisha mabadiliko ya sheria hiyo, wakisema yanaweka mwanya wa upendeleo, ukabila na hila, gazeti la Metro limeripoti.
Chama cha Wanasheria cha Kenya (LSK) kilifungua kesi hiyo kikipinga mabadiliko ya sheria sehemu ya 30 (3) yaliyofanywa na Bunge Desemba mosi mwaka jana na kusainiwa na Rais Uhuru Kenyatta kabla ya Krismasi, kwa maelezo kuwa yanapingana na Ibara ya 166 ya Katiba.
Mabadiliko hayo yalitaka Tume ya Huduma ya Mahakama (JSC) kuwasilisha kwa Rais majina matatu katika kila nafasi ya watu wanaopendekezwa kuteuliwa kuwa Jaji Mkuu na Naibu Jaji Mkuu.
LSK ilisema mabadiliko hayo yanaiondolea JSC uhuru wake wa kuteua mkuu wa mhimili huo wa nchi.
WATANZANIA WAWILI WATAJWA JARIDA LA FORBES
Watanzania wawili, Edwin Bruno na Nuya Hellen Dausen wametajwa katika jarida la Forbes Afrika kama wajasiriamali wenye umri wa chini ya miaka 30, wanaopewa kipaumbele kuwa mabilionea siku za usoni.
Kila mwaka jarida hilo hutoa orodha ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 30, wajasiriamali ambao wana nafasi ya kuwa mabilionea hapo baadaye.
Bruno ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Smart-code inayotoa huduma ya usomaji wa magazeti kwa njia ya mtandao, ametajwa katika jarida la Forbes Afrika mwaka huu.
Nuya, aliyewahi kuwa Miss Universe ni Mkurugenzi Mtendaji wa Nuya Essence, kampuni inayotengeneza bidhaa za ngozi na vipodozi.
VIJANA 30 MAARUFU KAMA “TEREZA”WALIOKUWA WAKIWABAKA NA KUWAJERUHI WANAWAKE WAKAMATWA
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limefanikiwa kudhibiti wimbi la wanawake kubakwa na kujeruhiwa na vijana wanaojulikana kama Tereza baada ya kuendesha msako na kuwakamata vijana 30 wanaotuhumiwa kuunda genge linaloendesha vitendo hivyo mitaani nyakati za usiku.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ferdinand Mtui amesema watu hao ambao wamekamatwa katika maeneo ya Vamia Mwanga na Katubuka watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika na kwamba wamebaini kuwa maeneo yanakotokea matukio hayo ya ubakaji hakuna umeme, nyumba nyingi hazina milango imara na maeneo hayo yamezungukwa na vilabu vya pombe.
Kwa upande baadhi ya wakazi wa mjini Kigoma,wamesema uwepo matukio hayo ya ubakaji umesababisha hofu katika jamii ambapo wamelitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi zaidi wa suala hilo na kulipatia ufumbuzi wa kudumu ili kuondoa hofu katika jamii.
Mauaji haya, serikali sasa itoe tamko
Mwezi huu wa tano tayari kuna matukio zaidi ya matano ya mauaji ya kikatili ya watu kuchinjwa au kukatwakatwa kwa mapanga.
Linaloshangaza wengi na kuibua maswali ni staili ya wauaji ya kuua bila kuchukua kitu chochote kutoka kwa wanaouawa jambo linalotia shaka kwamba huenda wauaji siyo majambazi.
Tukio la hivi karibuni ni la kuuawa kwa Aneth Msuya (30), aliyeuawa kwa kuchinjwa usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita Kigamboni jijini Dar es Salaam kisha waliofanya unyama huo wa kikatili kudaiwa kuondoka na televisheni.
Kama hilo halitosjhi, usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, watu wawili mume Saidi Somba (48) na mkewe Kadogo Ehicho (47), waliuawa kikatili katika Kijiji cha Mmazani wilayani Butiama, mkoani Mara kwa kukatwa na mapanga wakiwa kwenye nyumba yao.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mmazami, Jackson Kitukuru“, waliotenda unyama huo walichukua simu ya mkononi aina ya Tecno na wakatokomea kusikojulikana.
Mei 19,mwaka huu watu 15 wakiwa wameficha nyuso zao walivamia msikiti katika Mtaa wa Utemini wilayani Nyamagana, Mwanza na kuwaua watu watatu waliokuwa wakiswali usiku kwa kuwakatakata mapanga na shoka.
Mashuhuda walisema kwamba wauaji hao walidai hatua hiyo ilitokana na kitendo cha waliouawa kuswali wakati wenzao wanashikiliwa na polisi.
Mwezi huuhuu, watoto wanne wa familia moja inayoishi Kijiji cha Msufini, Kata ya Ndungu wilayani Same, Kilimanjaro waliuawa kwa kukatwakatwa mapanga wakiwa wamelala baada ya kuvamiwa na mtu aliyedaiwa kuwa ni ndugu yao na baba wa watoto hao akasema kwamba hajafahamu sababu ya kufanya ukatili huo kwani hawakuwa na ugomvi naye.
Tukio lingine lililotokea mwezi huu ni lile la watu saba wa familia moja kuuawa wilayani Sengerema mkoani Mwanza, nao waliuawa kwa kukatwakatwa na mapanga na watu wasiojulikana.
Lakini pia wiki iliyopita askari wa usalama barabarani, Ally Kinyogoli aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake.
Hakika matukio hayo yanatishia usalama wa raia na mbaya zaidi hatujasikia kauli ya serikali ya kulaani mauaji haya ambayo yamekithiri na kuwatia hofu wananchi kwani wanaouawa ni watu ambao hawana hatia.
Mimi nilitegemea wizara ya mambo ya ndani ingetoa kauli kupitia Bunge linaloendelea sasa katika jengo lake mjini Dodoma.
Kwa kweli ukimya huu wa serikali unawafanya wananchi kila mmoja kuwa na mawazo yake kichwani na tayari wengi wanaweza kufikiria njia mbadala za kujihami jambo linaloweza kuhatarisha usalama wa nchi.
Nashauri serikali kupitia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yusuf Masauni itoe tamko bungeni sasa ili hali hii isizidi kuwapa hofu wananchi.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.
Wananchi: Mwanza Si Salama!
Marehemu Nyenzi.
Na Johnson James, UWAZI
MWANZA: Kufuatia kuuawa kwa kupigwa risasi kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bubale, Kata ya Buhongwa, Alphonce Mussa Nyenzi hivi karibuni, wananchi wa jiji hilo wameeleza wasiwasi wao wakidai sasa Mwanza si salama tena, Uwazi linakuhabarisha.
Maisha ya kiongozi huyo yalikatishwa baada ya kupigwa risasi na mtu asiyejulikana wakati akizungumza na wanandoa wawili njiani walioomba kusuluhishwa.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili, kwa kuomba hifadhi ya majina yao kwa ajili ya usalama, wamesema wanapata hofu, hasa baada ya kubaini kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la mauaji ambayo yanawatisha, kwani wanaouawa ni viongozi na wananchi.
Wakazi wa eneo la Bubale walisema tayari viongozi wawili wa mtaa huo, ambao wao wanawaona ni wazuri kwa sababu ya kusimamia sheria, wameuawa kwani kabla ya marehemu Alphonce, mtangulizi wake, Julius Kasabuku naye aliuawa.
Wawakilishi wa wenyeviti wa mitaa katika Wilaya ya Nyamagana wameliambia gazeti hili kuwa hali ya sasa jijini Mwanza inatishia amani, hivyo kuanzia msiba huo uliotokea, wataanza kufanya sensa ili watu wafahamike katika mitaa yao, lakini pia wakaiomba serikali kuboresha ulinzi wao, kwani hivi sasa wanatamani kujiuzulu nyadhifa zao kutokana na kuuawa.
Waombolezaji wakiaga mwili wa marehemu.
Jumla ya watu 12 wameuawa mkoani Mwanza Mei mwaka huu, saba kati yao wilayani Sengerema ambao ni wa familia moja, huku Ilemela na Nyamagana zikishuhudia mauaji mengine ya watu wanne katika Msikiti wa Rahmani Mei 19, mwaka huu, hali iliyomfanya Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula kuona hali si salama na kushangaa kuona hakuna tamko linalotolewa na serikali katika kudhibiti hali hiyo.
“Nashangaa kuona wizara ya mambo ya ndani imekaa kimya kuhusu mauaji haya na mimi niwaahidi wananchi kuwa nitakapofika bungeni, mwongozi wangu wa kwanza kwa spika utakuwa ni kuhoji kwa nini halijatolewa tamko kuhusu suala hili,“ alisema Mabula.
Katika tukio la msiba wa Alphonce Mussa, wakati mwili wa marehemu ulipowasili ukitokea Hospitali ya Sekeu Toure ulikokuwa umehifadhiwa, mzozo ulitokea baina ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vijana wanaoendesha pikipiki maarufu kama bodaboda, ambao walikuwa wakigombea kuupokea mwili huo na kuuingiza ndani ya nyumba yake.
Lakini baadaye wakakubaliana kuwa wanachama wenzake hao wauingize mwili huo ndani na vijana wa bodaboda watautoa tayari kuelekea makaburini. Ilipofika wakati wa kuutoa nje, vijana hao waliutoa nje, waliuzunguka na kufanya ibada fupi kabla ya wenyewe kuondoka eneo hilo.
Getruda Alphonce, ambaye ni mke wa marehemu, aliiomba serikali kuwasaka wauaji wa mumewe na kuwakamata, ili sheria ichukue mkondo wake.
“Ninamshukuru Mungu ninaendelea vizuri, kwani mara nilipopewa taarifa hizi presha yangu ilipanda sana, sitamuona tena mume wangu,” alisema mke huyo huku akitokwa machozi.
Marehemu aliyeacha watoto 15, tisa kati yao wakiwa wa kike, alizikwa wiki iliyopita Kwimba alikozaliwa.
Wanafunzi Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Wagoma
Wanafunzi wa chuo kikuu cha cha Dar es salaam mpaka sasa wamegoma wakiishinikiza bodi ya mikopo kutoa fedha kwa ajili ya kujikimu.
Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi, Shamila Mshengema amesema mgomo huo ni matokeo ya taarifa zisizoeleweka zilizo kuwa zikitolewa na bodi juu ya lini fedha hizo zitatolewa.
Kwa kawaida pesa ya chakula huingiziwa kila baada ya siku 60 na mpaka sasa yapata wiki mbili pesa hiyo haijaingizwa.
Mgomo huo unakuja zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya Rais Magufuli Kuzulu chuo hicho kwa ajili ya uzinduzi wa jengo la Maktaba.
Kitilya na wenzake wazidi kusota Mahakama ya Rufaa Dar
Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya akienda kupanda gari litakalompeleka rumande.
LEO katika Mahakama ya Rufaa Tanzania, jijini Dar es Salaam Kamishna Mkuu mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake waliokuwa wafanyakazi wa Benki ya Stanbic Tanzania, Sioi Sumari na Shose Sinare walifikishwa mahakamani hapo kusikiliza rufaa iliyokatwa na upande wa Jamhuri.
Jamhuri imekata rufaa kupinga kufutwa shitaka namba 8 linalowakabili wote kwa pamoja la utakatishaji fedha linalowakabili. Hata hivyo, mahakama hiyo itapanga tarehe ya kusikilizwa shauri hilo siku itakayotangazwa.
Washitakiwa hao wanakabiliwa na shitaka la kula njama na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kinyume na sheria na walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Aprili Mosi, mwaka huu wakikabiliwa na mashtaka nane likiwamo la utakatishaji wa dola za Kimarekani milioni sita ambazo ni sawa na zaidi ya Sh bilioni 12.
Mashtaka yao yanatokana na tuhuma za ufisadi ulioipotezea serikali zaidi ya Sh. trilioni 1.3 katika kipindi cha kati ya mwaka 2012 na 2013 za uuzaji wa hati fungani.
PICHA NA HABARI NA DENIS MTIMA
Dada wa Msuya Kuchinjwa… Mchezo ni Huu
Jeneza lenye mwili wa marehemu.
Na Waandishi Wetu, UWAZI
DAR ES SALAAM: Bado habari ni moto! Majonzi yanaendelea kutawala kwenye familia ya Bilionea Erasto Msuya (43) aliyeuawa kwa kupigwa risasi Agosti 8, 2013, Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (Kia) kufuatia safari hii, mdogo wake wa kike, Aneth Simon Msuya (30) naye kuuawa kwa kuchinjwa shingo na watu wasiojulikana, Uwazi limebaini mchezo mzima.
Aneth (pichani) alifanyiwa ukatili huo, Mei 26, mwaka huu chumbani, nyumbani kwake, Block 16, Kibada- Kigamboni jijini Dar es Salaam akiwa na mtoto wake, Allan Kimario.
Mauaji hayo yaligunduliwa na jirani asubuhi baada ya mtoto wa marehemu, Allan kwenda kusema mama yake haamki na yeye anataka kwenda shule huku basi la shule likiwa limemwacha. Pia alisema anahisi njaa.
Jirani huyo aliongozana na mtoto huyo hadi ndani na kuubaini mwili huo ukiwa umalala sakafuni kwenye dimbwi la damu na kisu kilichotumika kumchinjia kikiwa pembeni yake na hivyo kutoa taarifa polisi.
Tangu kutokea kwa tukio hilo, vyombo mbalimbali vya habari nchini vimekuwa vikiripoti tukio hilo katika njia za kusikitisha sana kutokana na unyama aliofanyiwa Aneth na ndipo, Uwazi nalo likazama mitaani kuchimba kwa kina ili kuwapa wasomaji wake mambo mapya zaidi.
Madai yaliyosambaa ni kwamba, kuna kundi la watu limepanga mkakati mzito wa kuhakikisha familia ya Msuya inafutika kwenye uso wa dunia kutokana na kisasi cha kibiashara (bila kufafanuliwa).
“Ilivyo ni kwamba, baada ya kaka yao (Erasto) kuuawa, kwa kupigwa risasi, kuna kundi la watu limeamua kuifuta familia hiyo kwenye uso wa dunia. Ndiyo maana mbali na Aneth kuchinjwa, kuna akina Msuya wengine wameshakumbana na vitendo vya kuashiria kwamba, roho zao zinasakwa
Kwa mujibu wa chanzo kimoja toka ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania, msichana anayedaiwa kufanya kazi za ndani ‘hausigeli’ nyumbani kwa marehemu Aneth na kuondoka siku ya mauaji hayo, anapewa nafasi ya kwanza katika kuchunguzwa akisemekena kuujua mchezo mzima wa kifo cha bosi wake huyo na sasa jeshi hilo linamsaka kwa udi na uvumba.
“Kwanza nataka kusema kuwa, hausigeli ndiye mshukiwa wetu wa kwanza ndani ya jeshi la polisi. Huyu msichana wa kazi aliondoka mchana, usiku yakatokea yaliyotokea, akipigiwa simu hapatikani.
“Huyu tunamtuhumu kuujua mchezo wote. Kwa hiyo pa kuanzia kwetu tunafanya juu chini kumpata ili aisaidie polisi,” kilisema chanzo hicho huku kikiomba hifadhi ya jina kwa vile, si msemaji sahihi wa jeshi hilo.
ALIPANDIKIZWA?
Pia, chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa, utafiti wa awali wa jeshi hilo unataka kukubaliana kwamba, kutokana na mlolongo unaotokea wa mauaji au kujeruhiwa kwa watu mbalimbali wa familia ya Msuya, kuna uwezekano msichana huyo wa kazi alipandikizwa na watu hao kufanya kazi kwa Aneth.
“Kuna wasiwasi yule dada wa kazi alipandikizwa. Kuna uwezekano alifika pale katika njia za mtego ili kumsoma Aneth na mazingira yake pamoja na mwenendo, sasa baada ya kukamilisha ndiyo akaamua kuondoka na usiku wauaji wakafika. Kwa hiyo hayo yote sisi polisi tunayachunguza,” kilisema chanzo.
WAUAJI WALIINGIAJE NDANI?
Kwa mujibu wa chanzo hicho, inaaminika kwamba, wauaji hao walifanikiwa kuzipata funguo halisi za geti kubwa la mlango wa kuingilia sebuleni kwa Aneth, wakaenda kuchongea nyingine ambazo siku walipofika, waliweza kufungua geti na kuingia kama kwao.
“Lile geti kubwa linafunga kwa nje na funguo, kwa ndani unavuta loki tu. Kwa hiyo wao waliingia ndani kwa kufungua. Walipomaliza kutenda ukatili wao, inaonekana walifunga geti kubwa kwa kuloki ambapo kwa mtu mwingine wa nje asingeweza kuingia ila yule mtoto (Allan) aliweza kutoka nje kwa sababu loki yake ni ya kubetua tu.”
KWA NINI WAUAJI WALIIBA TIVII TU?
Chanzo hicho kikasema kuwa, watuhumiwa hao hawakuiba kitu zaidi ya tivii (flat) lakini inaonekana kwamba waliamua kuichukua runinga hiyo kwa vile waliamini ni skrini kwa ajili ya kamera za ulinzi (Closed-Circuit Television au CCTV) ambapo walijua picha zao zilichukuliwa. Hata hivyo, tivii hiyo waliitupa mbele ya safari.
HAIKUWA RAHISI KUMCHINJA ANETH
Chanzo hicho kilisema kuwa, mazingira ya chumba yalionesha kuwa, kabla ya kuchinjwa, kulikuwa na purukushani kubwa kwani neti ilikutwa imechanwa, baadhi ya vitu vimepinduliwa, vingine vimezagaa kila mahali hali ambayo iliashiria kuwa, marehemu hakukubali kuchinjwa kirahisi.
MAISHA YA ANETH
Baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili wakidai kumjua dada huyo, walisema kuwa, baada ya kifo hicho wamebadili mawazo kuhusu yeye kuwa huenda alijua anawindwa.
“Awali tulijua ni dada anayeringa, kwani alikuwa akifika dukani, anaegesha gari jirani kabisa na mlango wa duka kisha anaagiza kitu anachokitaka, anapelekewa, analipa pesa anaondoka.
“Hata siku tatu kabla ya kifo, alifika kwenye kibanda cha chipsi, akaagiza na kufungiwa akiwa ndani ya gari. Alikuwa hana kawaida ya kushuka, huenda alijua anawindwa,” alisema mkazi mmoja wa maeneo ya Kibada huku akiomba hifadhi ya jina lake.
SIMU ZA KUULIZWA ALIPO
Mmoja wa watu waliodai kufanya kazi na marehemu wizara ya fedha, alisema kuwa, wiki chache nyuma, Aneth aliwahi kusema kuwa, kuna wanaume wamekuwa wakimpigia simu na kumuuliza; Aneth uko wapi?’ lakini akiuliza we nani? Simu inakatwa!
“Huenda wale watu nao si sehemu ya watuhumiwa hawa. Maana hali hiyo alisema hakuwahi kukumbana nayo siku za nyuma. Baada ya kusikia amechinjwa sasa nahisi huenda Aneth alifuatiliwa kwa siku nyingi nyuma lakini yeye alikuwa hajui,” mtu mmoja aliliambia Uwazi kwa kumkariri mfanyakazi mmoja wa wizara hiyo.
MAISHA YAKE NA MAJIRANI
Baadhi ya majirani na nyumba ya marehemu walisema kuwa, haikuwa rahisi kubaini mienendo ya watu wasioeleweka nyumbani kwa Aneth kwa vile maisha yake yalikuwa hayasomeki kwa mwanga wa kawaida.
“Alikuwa akikuona anakusalimia akiwa ndani ya gari, akiingia kwake ameingia. Sasa isingekuwa rahisi kumjua kwa undani yeye na wageni wanaofika kwake. Lakini mimi nimewahi kusikia kwamba, Aneth aliolewa ila kwa bahati mbaya ndoa yake ilivunjika mwaka mmoja na baba wa mtoto wake,” alisema jirani mmoja kauli ambayo pia ilithibitishwa na dada mmoja wa Aneth.
NDUGU WASHTUKA, WAWEKA MLINZI
Gazeti la Uwazi pia lilifanikiwa kufika nyumbani kwa marehemu ambapo lilikuta nyumba inalindwa na mlinzi ambaye alisema aliwekwa hapo baada ya mauaji hayo.
UWAZI OFISINI KWA RPC TEMEKE
Hayo yote yalikuwa maneno mbalimbali ya vyanzo vyetu, hivyo mwishoni mwa wiki iliyopita, Uwazi lilifika ofisini kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, ACP Gilles Mroto ili kumsikia kama ana mtiririko huo, lakini kwa upande wake, alisema kuwa, wapo katika msako mkali kuwasaka wauaji hao.
“Hata huyo hausigeli pia tunamsaka sana ili kulisaidia jeshi la polisi kwa vile uondokaji wake na mauaji kuna utata,” alisema Kamanda Mroto.
MATUKIO YA KUIANDAMA FAMILIA
Tangu kutokea kwa mauaji ya Erasto, kumekuwa na matukio mengi ya kuiandama familia hiyo kwa kutaka kuwatoa roho wahusika.
KUNA ALIYEMWAGIWA SUMU
Dada wa Aneth aliyetajwa kwa jina la Antuja aliwahi kumwagiwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni sumu wakati akiwa amelala chumbani na mtoto wa Aneth, Allan hivyo kuathirika na sumu hiyo.
TUKIO LA HONGERA BAR
Desemba mwaka jana, dada mwingine aitwaye Ester na muwewe walipigwa risasi mgongoni na kifuani wakiwa katika Baa ya Hongera, Kijitonyama, Dar.
Mwili wa Aneth alisafirishwa jana kwenda Kijiji cha Kairo, Mererani, Simanjiro, Manyara kwa mazishi. Mungu aiweke pema peponi, roho yake. Amina.
[VIDEO] Kenyan woman in Houston responds to DJ Creme’s assertion that he was snitched on
Posted by Jambo
A Kenyan woman in Houston is responding to DJ Creme’s claim that he was snitched on leading to his immigration woes in the US.
Betty Achapa is disputing the claim of a snitch stating that she believes DJ Creme was a victim of his social media postings. She believes for a fact that no snitching happened and that it was all DJ Creme’s doing.
Here is her video.
RELATED STORY: [VIDEOS] DJ Creme gives details of his imprisonment in US
RELATED STORY: I went through an ordeal I would never want to relive ever again – DJ Creme after heading back to Kenya
RELATED STORY: I went through an ordeal I would never want to relive ever again – DJ Creme after heading back to Kenya
Mke wa Trafiki Kinyogori Adaiwa Kukiri Kumuua Mumewe
MKE wa askari polisi wa kikosi cha usalama barabarani (trafiki), Sajenti Ally Salum (Kinyogori) aliyeuawa hivi karibuni, inadaiwa amekiri kuhusika kwenye mauaji hayo, akidai ilitokana na mumewe kumuacha na kuoa mke mwingine. Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mwanamke huyo anashikiliwa na polisi kwa mauaji hayo yaliyofanyika...
Symbion Yaionya TANESCO.....Yasema Maneno ya Kizushi na Ukiukwaji wa Mkataba Wanaoufanya Utaligharimu Taifa
Kampuni ya kufua umeme ya Symbion imesema maneno ya uzushi na ukiukwaji wa mikataba unaofanywa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) utaligharimu Taifa na kulitaka shirika hilo kusema ukweli kuhusu makubaliano yao. Kampuni hiyo pia imeeleza kuwa mwishoni mwa mwaka jana, kigogo mmoja wa Tanesco (ametajwa jina lakini tunalilisitiri jina lake kwa sababu hakupatikana jana) alisaini mkataba...
14 Mbaroni kwa Tuhuma za Ujambazi
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu 14 wakiwamo wanawake wawili na mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mwika wilayani Moshi, kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha. Miongoni mwa watuhumiwa hao wapo wanaodaiwa kuwa majambazi sugu 10, waganga wa kienyeji wawili ambao walikuwa wakitumika kwa ajili ya kuwapa dawa watuhumiwa hao ili wasikamatwe na polisi na...
Chura ya Snura Yauzwa Kama Njugu!
STORI:WAANDISHI WETU, WIKIENDA
DAR ES SALAAM! Majanga! Wimbo wa Chura wa msanii anayekuja juu kwa kasi, Snura Mushi licha ya kusitishwa matumizi yake kwa kupigwa marufuku kusikilizwa hadharani au kuonesha video yake, sasa wajanja wametoa CD yake na inauzwa mfano wa njugu mitaani, kwa Sh. 4,000, Wikienda limeinasa.
DAR ES SALAAM! Majanga! Wimbo wa Chura wa msanii anayekuja juu kwa kasi, Snura Mushi licha ya kusitishwa matumizi yake kwa kupigwa marufuku kusikilizwa hadharani au kuonesha video yake, sasa wajanja wametoa CD yake na inauzwa mfano wa njugu mitaani, kwa Sh. 4,000, Wikienda limeinasa.
Mei 4, mwaka huu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliifungia video ya wimbo huo kwa madai kwamba haiendani na maandili ya Kibongo huku Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) likimtaka msanii huyo kuurekebisha wimbo huo na yeye mwenyewe kujisajili kwenye baraza hilo ili aweze kutambuliwa.
WIKIENDA LATONYWA
Wiki mbili zilizopita, baadhi ya wasomaji wa Wikienda walipiga simu chumba cha habari na kuuliza kama video ya Wimbo wa Chura imeruhusiwa kuuzwa au kuoneshwa madukani, kwani kumbukumbu zao, ulizuiwa na hakuna maamuzi ya kinyume na zuio hilo.
Wiki mbili zilizopita, baadhi ya wasomaji wa Wikienda walipiga simu chumba cha habari na kuuliza kama video ya Wimbo wa Chura imeruhusiwa kuuzwa au kuoneshwa madukani, kwani kumbukumbu zao, ulizuiwa na hakuna maamuzi ya kinyume na zuio hilo.
Wikienda: “Ile video bado ipo ndani ya zuio, kwani vipi kaka?”
“Sasa mbona CD (VCD) inauzwa mitaani, tena mbaya zaidi si mtaani tu hata kwenye baadhi ya maduka ya Kariakoo pia inauzwa,” alisema msomaji huyo aliyesema anaishi Kimara Suka, Dar. Siku tatu nyuma, msomaji mwingine alipiga simu na kusema makazi yake ni Mabatini jijini Mbeya
naye alisema habari kama hizo, kwamba, Video ya Chura ameiona ikiuzwa kwa siri mitaani.
“Sasa mbona CD (VCD) inauzwa mitaani, tena mbaya zaidi si mtaani tu hata kwenye baadhi ya maduka ya Kariakoo pia inauzwa,” alisema msomaji huyo aliyesema anaishi Kimara Suka, Dar. Siku tatu nyuma, msomaji mwingine alipiga simu na kusema makazi yake ni Mabatini jijini Mbeya
naye alisema habari kama hizo, kwamba, Video ya Chura ameiona ikiuzwa kwa siri mitaani.
WIKIENDA LAFANYA UTAFITI
Kufuatia taarifa hivyo, timu ya Wikienda ilizama mitaani na madukani, hasa Kariakoo ili kujiridhisha na madai hayo mazito. Kweli, katika baadhi ya maduka ya kuuza tv Kariakoo, Wikienda lilishuhudia video hiyo ikioneshwa kwenye ‘flat screen’ kubwa huku baadhi ya wapiti njia wakiwa wamepiga kambi kuiangalia huku wakizozana juu ya wimbo wenyewe. Wapo waliotaka itolewe kwa kuwa ilishapigwa marufuku.
Kufuatia taarifa hivyo, timu ya Wikienda ilizama mitaani na madukani, hasa Kariakoo ili kujiridhisha na madai hayo mazito. Kweli, katika baadhi ya maduka ya kuuza tv Kariakoo, Wikienda lilishuhudia video hiyo ikioneshwa kwenye ‘flat screen’ kubwa huku baadhi ya wapiti njia wakiwa wamepiga kambi kuiangalia huku wakizozana juu ya wimbo wenyewe. Wapo waliotaka itolewe kwa kuwa ilishapigwa marufuku.
Baadhi ya watu waliokuwa wakitoka kwenye duka moja Kariakoo walisikika wakilaani kuoneshwa kwa wimbo huo wakisema kuwa, kama ilipigwa marufuku hakukuwa na sababu ya msingi ya wauza CD hao kuionesha video hiyo kwani ni kukaidi agizo la serikali.
CD YAPATIKANA SINZA
Wikienda liliendelea kufanya uchunguzi wake ambapo liliweza kuipata CD hiyo kwa muuzaji mmoja aliyekuwa akipitisha bidhaa zake nje ya Baa ya Way Side.
Wikienda liliendelea kufanya uchunguzi wake ambapo liliweza kuipata CD hiyo kwa muuzaji mmoja aliyekuwa akipitisha bidhaa zake nje ya Baa ya Way Side.
WIKIENDA NYUMBANI KWA SNURA
Ili kumsikia Snura mwenyewe anasema nini kuhusu ishu hiyo, Wikienda lilifunga safari hadi nyumbani kwake, Mwananyamala jijini Dar na kuzungumza naye kwa kina kuhusu kuwepo kwa biashara hiyo na kama kuna mkono wake. Kwanza, Snura alionekana kushangazwa sana na kitendo
hicho ambapo alisema hakuwa anajua, lakini akaanika anachokijua yeye.
Ili kumsikia Snura mwenyewe anasema nini kuhusu ishu hiyo, Wikienda lilifunga safari hadi nyumbani kwake, Mwananyamala jijini Dar na kuzungumza naye kwa kina kuhusu kuwepo kwa biashara hiyo na kama kuna mkono wake. Kwanza, Snura alionekana kushangazwa sana na kitendo
hicho ambapo alisema hakuwa anajua, lakini akaanika anachokijua yeye.
“Mimi nilitii agizo la Basata na ndiyo maana hata kwenye YouTube niliifuta, ila wajanja waliiwahi kuichukua na kupiga pesa kupitia mgongo wangu. “Watu wakikamatwa huko na polisi mimi simo, maana Chura nimeshamfungia ndani, sasa wao wanaendelea kumuhangaisha awape majanga, naomba nisiunganishwe maana sijui lolote.
“Najua wengi walibani (kuchoma) CD hivyo wanapiga pesa kupitia kazi yangu na hao wanaoitana Chura waache mara moja maana nimesikia wengine wamekamatwa na polisi kwa kuitana Chura,” alisema Snura.
KIONGOZI WA BASATA
Kufuatia sekeseke hilo, juzi gazeti hili lilimtafuta Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mungereza ambaye simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
Kufuatia sekeseke hilo, juzi gazeti hili lilimtafuta Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mungereza ambaye simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
YALIYOTOKANA NA YATOKANAYO
Kufuatia wimbo huo kuzua sintofahamu kutokana na wanenguaji wake wanavyocheza na maumbo yao, baadhi ya vijana wa kiume wakaanzisha utani wa kumwita mwanamke yeyote Chura jambo ambalo si la kiungwana hivyo, Mei 26, mwaka huu, Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala liliwataka wanawake kutoa taarifa vituo vya polisi wanapoitwa Chura na vijana pale wanapopita kwenye mitaa yao.
Kufuatia wimbo huo kuzua sintofahamu kutokana na wanenguaji wake wanavyocheza na maumbo yao, baadhi ya vijana wa kiume wakaanzisha utani wa kumwita mwanamke yeyote Chura jambo ambalo si la kiungwana hivyo, Mei 26, mwaka huu, Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala liliwataka wanawake kutoa taarifa vituo vya polisi wanapoitwa Chura na vijana pale wanapopita kwenye mitaa yao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Lukas Mkondya alisema jijini Dar hivi karibuni kuwa, jeshi lake halijapokea malalamiko lakini kama kweli mambo hayo yapo basi aliwataka vijana kuacha mara moja tabia ya kuwaita wanawake Chura na wale watakaoitwa kutoa taarifa.
Imeandaliwa: Hamida Hassan, Mayasa Mariwata na Gladness Mallya.
Imeandaliwa: Hamida Hassan, Mayasa Mariwata na Gladness Mallya.
MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA ANNETH MSUYA
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina (CP), Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha) juu ya Jeshi lake kuendelea na operesheni mbalimbali jijini Dar es salaam leo.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina (CP), Simon Sirro akionyesha silaha mbili aina ya bastola, zilizokamatwa katika Matukio ya Uhalifu jijini Dar leo.
Hasheem Thabeet atua Dar kimya kimya
Idris Sultan akimuonesha kitu Hasheem wakiwa kwenye tamasha la Nyama Choma Jumamosi iliyopita
Akiwa NBA Hasheem alichezea timu nne tofauti zikiwemo Memphis Grizzlies (2009 – 2011), Houston Rockets (2011–2012), Portland Trail Blazers (2012) na Oklahoma City Thunder (2012–2014).
Pia amechezea timu zingine za ligi ya chini, D-League Dakota Wizards, Rio Grande Valley Vipers na Grand Rapids Drive.
Katika misimu yote tisa aliyowahi kucheza, Hasheem alikuwa na wastani wa pointi 2.2, 2.7 rebounds, na 0.8 blocks kwa kila mchezo. Tafsiri yake ni kuwa mchezaji huyo hakuwa na mafanikio sana kwenye ligi hiyo
[VIDEO] The Harvard University graduate’s speech that has captivated America
Posted by Jambo
It’s the speech Harvard University is calling “the most powerful, heartfelt” speech “you will ever hear.”
Donovan Livingston, a master’s graduate at the university, was chosen by a committee of faculty, staff and students to speak at the School of Education’s convocation, a rep for Harvard told ABC News.
Instead of a traditional speech, Livingston used spoken word to perform his poem, “Lift Off.”
Livingston told ABC News that the “true inspiration behind the piece” was the fact that he couldn’t perform a poem when he gave his commencement remarks during his senior year of high school.
“The teacher who was in charge…threatened to take me offstage or cut my microphone when she caught wind that I wanted to incorporate a poem,” he recalled. “She wanted it to be traditional. So I complied, but I really wanted to address my class in my most authentic voice, which is what I said onstage Wednesday.”
The poem spoke about racial inequalities in the educational system, what it means to be black at Harvard and inspired the class of 2016 to use their roles as future educators to help others realize their full potential.
Livingston told his fellow classmates in part:
“I’ve been a black hole in the classroom for far too long;
Absorbing everything, without allowing my light to escape.
But those days are done. I belong among the stars.
And so do you. And so do they.
Together, we can inspire galaxies of greatness
For generations to come.
So no, sky is not the limit. It is only the beginning.
Lift off.”
Absorbing everything, without allowing my light to escape.
But those days are done. I belong among the stars.
And so do you. And so do they.
Together, we can inspire galaxies of greatness
For generations to come.
So no, sky is not the limit. It is only the beginning.
Lift off.”
The speech has been seen by more than 5 million people and was even shared by Justin Timberlake and Hillary Clinton.
Livingston — who hopes to become a faculty member or an administrator at a university one day — said he did not expect to get a standing ovation, nor did he expect the speech to go viral.
“My wife kind of did,” he admitted. “But I didn’t know it would be so well received. Whenever you put yourself out there especially with poetry, you’re making yourself vulnerable. However it was received, I would’ve felt great at the end of the day because I was being myself, but the fact that it blew up the way it did is a humbling experience.”
Livingston now plans to support his wife Lauren as she enters her second year of medical school at Wake Forest University and start his PhD program at the University of North Carolina at Greensboro this fall.
It makes sense for the son of two educators: His father is a retired principal and his mother is a speech pathologist, working with special needs students.
“I’ve always been around education, but I didn’t know it was something I was really passionate about until I got to college and looked around and saw … that everything I did catered to college access [and] college success. It felt natural,” the Winston-Salem, North Carolina, resident said. “I’m just really happy to carry on the legacy of my mother and father and I’m just grateful to walk in their footsteps.”
Read the transcript of his speech is here
I went through an ordeal I would never want to relive ever again – DJ Creme after heading back to Kenya
Posted by Jambo
By Jambonewspot reporter
DJ Creme de la Creme is at a loss as to what happened resulting in him being denied entry into the United States.
The DJ who real name is George Njuguna was denied entry into the US at the Dallas Fort-worth (DFW) International Airport on Wednesday before eventually heading back to Kenya on Thursday. (Read: After US Immigration hold, DJ Creme denied entry, placed on flight back to Kenya)
In a post on Instagram, DJ Creme said that he had gone through an ordeal he would never like to go through again.
“Been through an ordeal I’d never want to relive in my life,” he said referring to the debacle at the hands of the immigration authorities.
The master spinner started his post with a tinge of amusement writing “Dear Lord…who did this?”
He added that he will update Kenyans on exactly what transpired while at the hand os the US authorities terming his 25 hour ordeal as “prison break”
He ends his post assuring his US based Kenyan fans that he believes he will be able to join them some time soon. He wrote that he felt bad that it turned out the way it did.
“To my US family, I’m really feeling bad that it turned out this way, but everything happens for a reason and I know without a doubt that we shall party sometime soon,” he promised.
On Saturday night, he was spinning at the Blaze Kenya launch where he received rave reviews.
Subscribe to:
Posts (Atom)